More details

Mission & Evangelism

Makamu wa kwanza wa Mwenyekiti Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT, Baba Askofu Stanley Hotay( Kanisa Anglikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro) akiambatana na Katibu Mkuu wa CCT Mch.Canon.Dkt Moses Matonya pamoja na baadhi ya Viongozi wa CCT Mikoa na Wilaya wamekabidhi Rasmi Mahitaji muhimu ya waathirika wa mafuriko Kwa uongozi wa Serikali ya wilaya ya Hanang ,Mkoani Manyara. Mahitaji hayo muhimu yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni hamsini (50)vikiwemo simenti,mabati,nguo na vyakula vimekusanywa kupitia CCT mikoa na wadau mbalimbali wa CCT. Akikabidhi mahitaji hayo baba Askofu Stanley Hotay ameishukuru mikoa ya CCT ,wadau mbalimbali na watumishi wa CCT waliotoa mahitaji hayo kwa ajili ya waathirika wa mafuriko pia amesisitiza uongozi wa Serikali kuhakikisha mahitaji hayo yanawafikia walengwa kwa uaminifu kama ilivyolengwa Akipokea mahitaji hayo Mhe. Janeth Mayanja Mkuu wa Wilaya ya Hanang amewashukuru viongozi wa CCT kwa namna walivoshirikiana na serikali tangu mafuriko yalipotokea ,haswa amewapongeza viongozi wa CCT wilaya ya Hanang kwa namna wanavoshirikiana katika mambo mbalimbali kwenye wilaya hiyo,pia ameahidi vitu vyote vilivyotolewa vitawafikia walengwa kwa uaminifu. Katika hatua nyingine Mhe. Janeth Sanya ameipongeza CCT kwa kuendelea kutekeleza Miradi mbalimbali na kutoa elimu ya saikolojia kwa waathirika wa mafuriko na ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika Miradi na kazi zote za kusaidia jamii zitakazokua zikiendelea wilayani, Hanang.