SIKU YA MAOMBI YA DUNIA KITAIFA FEB 28, 2026 MBEYA
MATHAYO 11:28-30
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha..
IFAHAMU CCT
Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo inajulikana kwa kifupi kama CCT (Christian Council of Tanzania), ni Taasisi mwavuli inayowakilisha Umoja wa Madhehebu ya Kikristo ya Kiprotes- tanti Tanzania. Kwa sasa CCT inaundwa na Makanisa mbalimbali Wanachama na Vyama vya Kikristo au vyenye mwelekeo wa kikanisa kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Taasisi hii ilianzishwa rasmi tarehe 23 Januari, 1934 kutokana na maono ya Wamisionari kutoka Kanisa Anglikana, Kanisa la Moravian na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri. Wamisionari hawa walipata maono ya kujenga umoja kati ya makanisa wanachama ambao utajihusisha na masuala mbalimbali ya kiimani, kimaendeleo na kijamii.. Muungano huu ulijulikana kwa jina la Kiingereza, Tanganyika Missionary Council (TMC).
Mnamo mwaka 1964 Mungu aliwapa maono watumishi wake Baba Askofu Stephano Reuben Moshi (Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania), Baba Askofu Theofilo Kisanji (Kanisa la Moravian Tanzania) na Baba Askofu Mkuu John Sepeku (Kanisa Anglikana Tanzania) kubadilisha usajili wa TMC kuwa Christian Council of Tanzania (CCT), jina linalotumika hadi sasa.
Idadi ya Makanisa yaliyopo chini ya CCT imekuwa ikiongezeka kutoka Makanisa matatu (3) ya mwanzo mwaka 1934 hadi kufikia makanisa ya Kiprotestanti kumi na mbili (12) yaliyopo mwaka 2024
MALENGO MAHSUSI YA CCT
- Kuimarisha mafundisho ya Neno la Mungu, huduma za Kiroho na Uinjilisti kwa watu wote
- Kuratibu na kuendeleza huduma jumuishi za Maendeleo endelevu kwa mwanadamu kiroho na kimwili.
- Kuimarisha chombo cha CCT katika kujitegemea Kiuchumi na Usimamizi wa Rasilimali Fedha, Vitu na Watu katika kuihudumia jamii yote.
DIRA na DHAMIRA
Dira ya CCT (CCT Vision)
Kuwa chombo cha Ki-ekumene cha Kikristo chenye kuleta maendeleo kamilifu na endelevu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.
Dhamira ya CCT (CCT Mission)
Kudumisha umoja katika mwili wa Kristo na kuunganisha nguvu katika kutatua changamoto na kutumia fursa zilizopo kuleta maendeleo kamilifu na endelevu kwenye jamii.
Fahamu
Huduma Zetu
Utume na Uinjilisti
Kuimarisha Umoja wa makanisa wanachama CCT, kusimamia watoto shuleni kupitia chombo cha UKWATA na vyuoni kupitia chombo cha USCF.
Maendeleo na Utetezi
Kazi ya utetezi, Elimu ya kisheria na msaada wa kisheria kwa wanajamii, Uchambuzi wa sera, Kutoa elimu ya Afya, usalama wa chakula na mabadiliko ya tabia nchi.
Uwekezaji
Kuimarisha miradi ya uwekezaji kama ujenzi wa majengo ya kupangisha, Huduma za bima,Kilimo kwa ajili ya kuimarisha taasisi kujitegemea.
Waliopokea Elimu ya Kisheria
Waliopata Msaada wa Kisheria
Idadi ya vocoba
Idadi ya Chaplaicnies
CCT Day ni siku maalumu iliyowekwa kikatiba kwa lengo la kukumbushana misingi na umuhimu wa umoja wa makanisa na vyama wanachama wa CCT katika ngazi zote. Aidha siku hii imewekwa madhubuti ili kukumbusha waumini mmoja mmoja umuhimu wa umoja na shughuli za Jumuiya kwa Kanisa na Jamii. Siku hii hutolewa sadaka maalumu ambayo kazi yake kubwa ni kuendeleza shughuli za kitume na kijamii zinazoratibiwa na CCT. Kwa mwaka huu, Maadhimisho ya CCT Day yatafanyika mwezi Mei na kilele chake kitakuwa Tarehe 31 Mei 2026 ambapo Kitaifa yataadhimishwa Mkoani Njombe. Aidha shughuli za Maadhimisho ya CCT Day yatafanyika katika mikoa yote nchini. Maadhimisho haya yatafanyika kwa kuwa na matukio mbalimbali yatakayoratibiwa na Kamati za CCT kwenye Mikoa. CCT inatoa wito kwa kila muumini kuchangia kwa kadiri ya Baraka za Mungu alizomjalia ili kufikia Malengo yake ya kujiimarisha kiuchumi kwa ajili ya kutekeleza shughuli zake za kitume na kijamii.Michango inaweza kutumwa kupitia:-
-
CRDB akaunti namba: 01J1081943800 Jina CCT GS SPECIAL/ . - MPESA 0743784347 Jina Jumuiya ya Kikristo Tanzania .
- Ofisi za CCT katika Mikoa .
Tumshukuru Mungu
Tumshukuru Mungu
Tumshukuru Mungu
- Tumshukuru Mungu.
- Tumshukuru Mungu.
- Tumshukuru Mungu
- Tumshukuru Mungu.
Tumshukuru Mungu
Tumshukuru Mungu
- Tumshukuru Mungu
- Tumshukuru Mungu
- Tumshukuru Mungu
Tumshukuru Mungu.
Tumshukuru Mungu
Tumshukuru Mungu
Tumshukuru Mungu.
- Tumshukuru Mungu.
- Tumshukuru Mungu.
- Tumshukuru Mungu.
IBADA
Management
VIONGOZI WETU

Mchg Can Dkt.Moses Matonya
Katibu Mkuu
Godlisten Moshi
Mkurugenzi wa Utawala naRasilimaliwatu

Clotilda Ndezi
Mkurugenzi wa Programu za Manendeleona Utetezi

Beatrice Dengenesa
Mkurugenzi wa Uwekezajina Mwanasheria

Michael Mtally
Mkurugenzi WAMA
Emma Mashauri
Mkurugenzi MWTC
Etanga Kajanja
Mhasibu Mkuu
Urio Ndekirwa
Afisa Mwandamizi Mipango Tathmini,Ufuatiliaji na Mafunzo

Grace Mayengo
Mkaguzi wa NdaniWADAU WETU
WasilianaNasi
Jumuiya ya Kikristo Tanzania
Anwani
P.O Box 1454 Btn 8th and 9th Road, Dodoma
Piga Simu
+255262324445
Barua Pepe
info@cct.or.tz